2 Juni 2024 - 15:36
Chile yajiunga kwenye kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni

Rais Gabriel Burich wa Chile ameatangaza kuwa, nchi yake itajiunga kwenye kesi ya Afrika Kusini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai dhidi ya binadamu huko Gaza.

Katika hotuba yake kwenye Bunge la nchi hiyo, Rais Burich ameeleza kusikitishwa sana na jinai dhidi ya binadamu huko Gaza, haswa dhidi ya wanawake na watoto. Rais wa Chile amelishutumu jeshi la Israel kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.

Rais wa Chile amesema, hatuwezi kuacha kuonyesha hasira zetu dhidi ya vitendo vipofu na visivyo na uwiano kabisa vya jeshi la Israel dhidi ya raia wasio na hatia, hasa wanawake na watoto wa Kipalestina. Hatua hizi zinahitaji majibu madhubuti kutoka kwa jamii ya kimataifa.

Rais wa Chile ameongeza kuwa: Kwa hiyo, pamoja na kupeleka misaada ya kibinadamu Palestina, kumrejesha nyumbani balozi wetu kutoka Israel tunajiunga na kesi  dhidi ya Israel iliyowasilishwa na Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ).Mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka jana 2023, Afrika Kusini iliwasilisha malalamiko katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu dhidi ya utawala wa Kizayuni kutokana na utawala huo kukiuka makubaliano ya kupigwa marufuku jinai za mauaji ya halaiki. Hadi sasa nchi kadhaa zikiwemo Mexico, Uturuki, Colombia, Nicaragua na Libya zimeumba kujiunga na kesi hiyo kwa ajili ya kuwatetea na kuwaunga mkono Wapalestina wa ukanda wa Gaza wanaouawa kila siku na utawala haramu wa Israel.

342/